Dkt.Jingu ashiriki Kongamano la China-Africa Women's Forum

NA MWANDISHI WETU
WMJJWM, CHINA

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.John Jingu ameshiriki Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano kati ya China na Africa katika masuala ya Usawa wa Kijinsia (China-Africa Women's Forum) Juni 29, 2023 hadi Julai 1,2023.
Kongamano hilo lililoandaliwa na 'All China Women Forum' na kufanyika jijini Changsha, Jimbo la Hunan nchini China lilikuwa na lengo la kuainisha fursa zilizopo China na Afrika kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hususani katika nyanja ya uvumbuzi na ujasiriamali. 
Sambamba na kongamano hilo, lililokuwa na Kaulimbiu isemayo "Pooling the strength of Chinese and African women, and jointly promoting comprehensive development", yalifanyika pia makongamano mengine madogo likiwemo kongamano la kilimo lenye lengo la kukuza na kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya wakulima kwa ushirikiano wa China na Afrika. 
Mpango huo utasaidia kuongeza kipato kwa ngazi ya kaya, hali itakayosaidia kupunguza masuala ya ukatili yatokanayo na kipato duni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news