Dkt.Yonazi aitaka jamii kuendelea kujiandaa kujikinga na maafa

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt.Jim Yonazi ameitaka jamii kujiandaa kila wakati ili kujikinga na maafa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt.Jim Yonazi akizindua Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa Juni 30, 2023 jijini Dodoma.

Ameyasema hayo Juni 30, 2023 jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja.

Dkt.Yonazi amesema kuwa, Tanzania kama nchi imepitia historia ya kukabiliwa na matukio ya maafa yatokanayo na majanga na milipuko ya magonjwa ya binadamu na wanyama hivyo ipo haja ya kuwa na mipango ya kitaifa inayoratibiwa vyema kuwezesha kubaini viashiria na kushirikishana taarifa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokea. 

Pia alibainisha kuwa,ufuatiliaji wa matukio yanayoweza kuathiri afya ya binadamu, wanyama na mazingira unatakiwa kufanyika kwa ufanisi kwa kuzingatia dhana ya Afya Moja kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja 2022 - 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jim Yonazi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa Juni 30, 2023 jijini Dodoma.

Dkt.Yonazi amesema, matukio hayo hutokea bila matarajio na huhitaji utambuzi wa mapema na kuchukua hatua za haraka za kukabili.  

“Tumejifunza kuwa ili kudhibiti matukio hayo, hatuna budi kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema na uratibu ili kudhibiti viashiria vya matukio yanayoweza kusababisha maafa kwa wakati,”amesisitiza.
Washiriki wa Hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa wakiafuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 30, 2023 Jijini Dodoma.

Alitumia fursa hiyo kuhimiza watendaji kujifunza kutoka kwa Nchi zilizoendelea katika mifumo ya aina hiyo kwa lengo la kuboresha masuala ya menejimenti ya maafa.
“Nimefurahi sana kuona kuwa kuna washiriki kutoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali,na wawakilishi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, na kwa kuwa hili ni toleo la kwanza, sasa nitoe wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kuwa katika nchi zote zilizoendelea hawa ndo wabeba mwenge wa Sayansi na Teknolojia, tafiti zinafanywa katika majeshi na baaada ya hapo huamishwa na hupelekwa katika matumizi mengineyo,”amebainisha Dkt.Yonazi. 

Sambamba na hilo alitoa wito kwa Vyuo vya Elimu ya Juu hususan Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kuendelea kutoa ushirikiano katika mtazamo wa kisayansi katika mambo yanayotatiza jamii na kuyatafutia ufumbuzi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akifafanua jambo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa wakiafuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 30, 2023 jijini Dodoma.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,(SUA) Profesa Raphael Chibunda, Makamu alisema mradi huo wa kuanzishwa kwa jukwaa shirikishi la kidijitali ulizunduliwa mwaka 2022,na kupitia mradi huu shughuli mbali mbali zimetekelezwa,na ili kuhakikisha kituo hiki kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa ambapo Chuo cha (SUA) kilitoa vifaa vya TEHAMA vya Mradi huo vyenye thamani ya shilingi milioni 42.3.
Afisa TEHAMA Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Alex Ndimbo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) kuhusu mfumo wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa unavyofanya kazi.

Awali akitoa taarifa ya Mradi huo, Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Alex Ndimbo alisema lengo la kuanzishwa kwa jukwa hili ni kuongeza wigo kwa Jamii kutoa Taarifa kwa mamlaka husika. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na namba ya dharura ya kupokea taarifa za maafa uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 30, 2023 jijini Dodoma.(Picha na OWM).

“Jukwaa hili linawakutanisha wataalam wote ambao wanasimamia sekta zinazohusiana na wanyama, binadamu na mazingira wakikutana pamoja na kuratibu tutapunguza matukio ambayo yataleta majanga katika Taifa letu, mfumo huu unaenda kuruhusu wananchi wa kawaida kabisa kutoa taarifa kwa Serikali au Idara husika moja kwa moja kutoka katika eneo la tukio kupitia namba 190 kwa baadhi ya mitandao ya simu,"alibainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news