Epukeni ramani za ajabu ajabu mitaani-Waziri Dkt.Mabula

NA ANTHONY ISHENGOMA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amewataka Watanzania kuhakikisha wanatumia ramani sahihi zinazotolewa na wizara yake ambazo zimethibitishwa na Mpima Ardhi Mkuu wa Serikali, kwani matumizi ya ramani holela hayana tija.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akipata ufafanuzi kuhusu shuguli zinazofanywa na Kitengo cha Hati cha Wizara yake jana alipofika Viwanja vya Sabasaba kujionea huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi katika Maonesho ya 47 ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Waziri Dkt.Mabula amesema, kumekuwa na ramani za ajabu ajabu zinazouzwa mitaani ambazo hazijathibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Upimaji na Ramani aliyeko Wizara ya Ardhi hivyo kawataka watanzania wanapotaka kununua ramani inayoonesha mipaka na utawala maeneo sahihi ya kupata ramani hizo ni Wizara ya Ardhi.

Wiziri Mabula alisema hayo Julai 7, 2023 alipofika katika viwanja vya Maonesho ya 47 ya Sabasaba alipotembelea banda la Wizara yake kujionea huduma zinazotolewa kwa wananchi wanaofika kupata huduma zinazopatika katika sekta ya ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akipata ufafanuzi kuhusu shuguli zinazofanywa na kampuni ya Hamidu City jana alipofika Viwanja vya Sabasaba kujionea huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi katika Maonesho ya 47 ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

‘’Kumekuwa na ramani nyingi zinauzwa lakini ukiangalia vipimo vyake au namna walivyotenga maeneo hayo ni tofauti na kumbukumbu zetu za upimaji na ramani hivyo watanzania tumieni fursa hii kama ukitaka kuchukua ramani ya eneo lako basi fika Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi upate ramani sahihi na iliyothibitishwa.’’aliongeza Waziri Mabula.

Waziri Mabula aliitaka Jamii kutambua kuwa Wizara yake ndiyo sehemu pekee hapa Nchini ya kupata ramani na si vinginevyo na hivyo na kuongeza kuwa watanzania wengi wanatumia ramani zisizo sahihi na wala hawajui pa kwenda kuchukua ramani izo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikabidhi hati kwa Bi. Yohana Mairo jana alipofika Viwanja vya Sabasaba kujionea huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi katika Maonesho ya 47 ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kiongozi huyo alichukua fursa hiyo kuwakumbusha wananchi ambao walikabidhiwa jana hati zao kutolimbikiza kodi ya ardhi akionya kuwa kulimbikiza kodi hiyo kunachangia wanachi wengi kushindwa kulipa kodi ya pango ala Ardhi.

‘’Unaweza kukuta gharama ya kulipa ni ndogo, lakini ukimaliza mwaka mmoja na mwingine bila kulipa kodi inakuwa kubwa hivyo niombe ninyi mnaochukua hati leo kuhakikisha mnalipa kodi ya ardhi kila mwaka, haipendezi wewe leo unalipa mwaka hujao haulipi unasubiri mwaka mwingine ukianza kulimbikiza kodi inakuwa ni shida,"alisema Dkt.Angeline Mabula.

Aidha,Waziri Mabula aliwakumbusha wananchi kuhusu msamaha wa riba ya kodi ya pango la ardhi uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Julai 31, 2022 hadi Aprili,21 mwaka huu lakini watu hawakutumia fursa hiyo kulipa kodi ya pango ardhi ndiyo maana akaendelea kusisitiza umuhimu wa kulipa hiyo kwani fursa hiyo haijitokezi mara kwa mara.

Waziri Mabula aliongeza kuwa Wizara yake inaenda kufanya kazi kubwa ya kurahisisha zoezi la upimaji ardhi nchini kwa kupunguza umbali wa vipimo vya upimaji kutoka Km. 40 hadi 20 ili kuongeza kasi ya upimaji lengo likiwa kuhakikisha nchi inapimwa kwa asilimia miamoja.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara yake wanaoshiriki Maonesho ya Sabasaba jana alipofika Viwanja vya Sabasaba kujionea huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi katika Maonesho ya 47 ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Waziri Mabula aliongeza kuwa zoezi hilo linaendelea kupitia Mradi wa Uboreshaji Milki za Watu Nchini na utapima Halmashauri 44 nchini na kupanga matumizi bora ya ardhi katika Halmashauri hizo.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inashiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 na inaendelea kutoa huduma za hati, kutatua changamoto kwa wananchi zilizopo, kutoa elimu kwa umma pamoja na kushirikiana na sekta binafsi kutoa huduma za ardhi kupitia maonesho hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news