Jecha Salum Jecha afariki

ZANZIBAR-Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amefariki dunia leo Julai 18, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt.Muhamed Dimwa, amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo hicho huku kikisisitiza huo ni msiba mkubwa kwa taifa.

Wakati huo huo, taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na familia ya marehemu ikiwa ni saa chache baada ya mwenyekiti huyo mstaafu kufariki dunia.

“Kwa masikitiko makubwa tunawatangazia msiba wa mzee wetu aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.Taarifa za mazishi tutawajulisha, familia haijapanga bado mazishi yatakuwa saa ngapi,” imeeleza taarifa hiyo.

Jecha alipata umaarufu mkubwa hasa baada ya kufuta matokeo ya urais ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mgombea mmoja kujitangaza mshindi kwa madai kwamba haukuwa huru na haki.

Hatua hiyo ya kufuta matokeo hayo iliibua mvutano mkali kati ya ZEC na Chama cha Wananchi (CUF) ambao walidai kuwa aliyafuta matokeo hayo ili kuipa ushindi CCM.

Hata hivyo baada ya kuondoka ZEC, jina la Jecha liliibuka tena 2020 alipojitokeza hadharani na kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea Urais wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news