Fisi aua mwanakijiji

MTWARA-Haika Mangeja (62) mkazi wa Kijiji cha Chiwambo katika Kata ya Lulindi wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara ameuawa baada ya kuvamiwa na fisi wakati akijaribu kumuokoa mke wake.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Maimuna Mbaya amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa saba usiku wakati Mangeja na mke wake, Asina Nguriko (49) wakiwa ndani ya nyumba yao wakiota moto na fisi huyo kuwashambulia.

Aidha, wananchi wa kijiji hicho walifika eneo la tukio na kumkuta fisi huyo akiwa anakula mwili wa marehemu eneo la kichwani na kumuua kwa kutumia silaha za jadi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news