JKCI kuja na dozi ya nguvu za kiume

DAR ES SALAAM-Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) inatarajia kuanza kutoa huduma ya kuzibua mishipa ya uume ikiwa ni hatua ya kukabiliana na upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wenye tatizo hilo.

Mkurugenzi wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge amewaeleza wanahabari leo Julai 27, 2023 jijini Dar es Salaam kuwa, huduma hiyo inatarajiwa kuanza mwezi Oktoba, mwaka huu.

Amesema, tatizo hilo ni kubwa japo hakuna utafiti walioufanya, lakini wapo wanaume wenye tatizo hilo wanafika katika taasisi hiyo.

“Tutakwenda kuanzisha huduma mpya ambapo tutashirikiana na wenzetu wa India, kwani tatizo la nguvu za kiume linazidi kuongezeka kwa mishipa ya uume kuziba.Tatizo lipo na pengine hilo ni siri ya wagonjwa hatuwezi kuweka wazi ila huduma itaanza mwaka huu,”amesema Dkt.Kisenge.

Amesema,tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni kubwa na linazidi kuongezeka kutokana na mishipa ya uume kuziba na hivyo mwanaume anashindwa kuhimili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news