Uwanja wa Benjamin Mkapa kufanyiwa ukarabati mkubwa

DAR ES SALAAM-Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam unatarajiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amesema, serikali imedhamiria kufanya hivyo ili kuufanya uwanja huo kuwa wa kisasa zaidi.

Ameyabainisha hayo leo Julai 27, 2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kwa ajili ukarabati huo.

Yakubu amesema shilingi bilioni 31.3 zitatumika kukamilisha ukarabati huo katika kipindi cha miezi 12 na utaendelea kutumika kama kawaida hadi pale ukarabati wa eneo la kuchezea utakapoanza.

Uwanja huo ambao upo Kata ya Miburani una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ambapo ulibuniwa na Kampuni ya WMS Architects kutoka Afrika Kusini na kujengwa na Beijing Construction Engineering Group miaka kadhaa iliyopita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news