Kiswahili ni kitega uchumi kinachojitosheleza-Profesa Lumumba

NA MWANDISHI WETU

PROFESA wa sheria na mtoa mihadhara maarufu kutoka Kenya,Patrick Lumumba amesema, ukitaka kuelewa lugha ni lazima kutambua muktadha wake na Kiswahili ni kitega uchumi ambacho kinajitosheleza kisayansi kwa maendeleo ya watumiaji wa lugha hiyo.

Prof. Lumumba amesema hayo Julai 5, 2023 jijini Zanzibar wakati wa mjadala wa wazi kuhusu "Kiswahili Nyenzo ya Ukombozi wa Fikra kwa Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika" ikiwa ni Kuelekea Kilele cha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, 2023.

"Kiswahili ni lugha ya Kiafrika, ni nyenzo pekee ya kuwakomboa Waafrika, kinatuunganisha sisi sote Waafrika, tujivunie Siku ya Kiswahili Duniani,"amesema Prof. Lumumba.

Kwa upande wake Prof. Amani Lusekelo ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema, Taasisi za Elimu ya Juu nchini zina wajibu wa kupanua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kuandika tasnifu kwa lugha ya Kiswahili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news