LIVE:Rais Dkt.Samia akimpokea mgeni wake Rais Novák

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Hungary, Mheshimwa Katalin Novák leo Julai 18,2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Novák aliwasili nchini usiku wa Julai 17,2023 kwa ziara ya kikazi ya siku nne itakayomalizika Juali 20, Julai 2023.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mheshimiwa, Novák alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.)

Aidha, leo Mheshimiwa Novák anatarajia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na baadae viongozi hao kuzungumza na waandishi wa habari.

Mheshimiwa Novák ni Rais wa kwanza mwanamke kuongoza Hungary ambapo alichaguliwa mwezi Mei, 2022. Aidha, ni Rais wa kwanza kutoka Hungary kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania.

Ziara hiyo ni matokeo ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, elimu, utalii, kilimo, utangazaji na viwanda.

Julai 17,2023 viongozi wengine walioambatana na Dkt.Tax kumpokea Rais wa Hungary ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Muliro Jumanne, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo,

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Tanzania nchini Hungary, Mhe. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme pamoja na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news