Mayele,Djuma,Bangala na Doumbia kwaheri Yanga SC!

DAR ES SALAAM-Huenda kandarasi ya Fiston Kalala Mayele, Djuma Shabani na Yanick Bangala katika Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imefikia tamati, hivyo kupewa mkono wa kwaheri.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inaonekana wameamua kufunga rasmi historia ya nyota hao kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya misimu miwili ya mafanikio tele.

Hayo yamebainika jioni ya leo Julai 22, 2023 baada ya Yanga SC kutambulisha wachezaji itakaowatumia katika msimu 2023/24 wa mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Watatu hao hawajatajwa katika kikosi cha msimu ujao na hiyo inawapa hisia mashabiki wengi kuamini kwamba huenda wamemalizana.

Mbali na hao pia Mamadou Doumbia kutoka nchini Mali hajatambulishwa kama sehemu ya kikosi hicho kupitia Siku ya Mwananchi leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news