Miradi ya maendeleo yamng'oa Mkurugenzi Mtendaji Buhigwe

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Angellah J. Kairuki (Mb) amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe mkoani Kigoma, ndugu Essau Hosiana Ngoloka, kuanzia Julai 11, 2023 ili kupisha uchunguzi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Nteghenjwa Hosseah ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa Kairuki, amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo, ukiwemo mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Kahimba ambayo ilipelekewa fedha shillingi bilioni moja.

Hata hivyo, mradi huo haujakamilika mpaka sasa wakati fedha zote zimeshatumika. Kutokana na tuhuma hizo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi amemwelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuunda timu ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na kuwasilisha taarifa kwake.

Aidha, Mheshimiwa Kairuki amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wote Nchini, kuendelea kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa utekelezaji wa miradi hiyo zinakamilisha miradi husika kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news