Waziri Dkt.Mabula ashiriki Mkutano wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ameshiriki Mkutano wa Pili wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe uliofanyika leo tarehe 13 Julai 2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akiwa na Mawaziri wenzake Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo na Deogratius Ndejembi Naibu Waziri TAMISEMIA katika Mkutano wa Pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.

Mkutano huo wa siku moja unaoongozwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu unahusisha viongozi na wataalamu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Malawi huku ujumbe wa Malawi ukioongozwa na Waziri wake wa Maji na Usafi wa Mazingira Mhe. Abida Sidik Mia.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.

Mawaziri wengine wa Tanzania wanaoshiriki mkutano huo ni Mhe. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu (Kushoto) akiwa na Waziri wa Maji wa Malawi M Abida Sidik Mia katika mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.

Mkutano huo ni muendelezo wa vikao vya pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na Malawi unaolenga kuimarisha usimamizi, uhifadhi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji ya mto Songwe.
Ujumbe wa Malawi ukiwa katika Mkutano wa Pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Malawi zilishiriki majadiliano ya pamoja yaliyofanyika mwaka 1976 kuhusu namna bora ya kutatua changamoto zinazosababishwa na Mto Songwe kwa madhumuni ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news