Mwinyi Zahera ndiye Kocha Mkuu wa Coastal Union

NA DIRAMAKINI

ALIYEWAHI kuwa kocha wa Yanga SC na Polisi Tanzania, Mkongo Mwinyi Zahera ametambulishwa kuwa Kocha mpya Mkuu wa Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Zahera anapewa kandarasi Coastal Union akitokea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa msaidizi wa Florent Ibenge tangu Septemba 30, mwaka jana.

Miongoni mwa timu ambazo Zahera amewahi kuzifundisha ni DC Motema Pembe ya kwao, DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016, akitoka kuwa kaimu kocha wa AFC Tubize ya Ubelgiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014 ambayo alijiunga nayo akitoka kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya Ibenge.

Alikuwa anafundisha AFC Tubize kwa mara ya pili, baada ya awali kuifundisha kama Kocha Mkuu kuanzia Julai 1 hadi Oktoba 20, mwaka 2010.

Zahera Mwinyi alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 mjini Goma kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa Jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.

Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka la kulipwa.

Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka.

Aidha, baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha, Zahera Mwinyi ambako alitunukiwa Diploma na leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kabla ya kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha Tubize na baadaye kutrejea nyumbani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news