NGOs kutoka Tanzania, China kufanya mdahalo

BEIJING-Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kutoka Tanzania na China yanatarajiwa kufanya mdahalo kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Rasilimali za Maji mwezi ujao jijini Zanzibar.

Mdahalo huo utafanyika kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Dubai Novemba, 2023.

Hayo yamebainishwa jijini Beijing nchini China wakati wa mkutano kati ya Rais wa Shirika lisilo la Kiserikali la China-Green Zhejiang,Hao Xin na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.

Kazi ya Green Zhejiang inajumuisha ufuatiliaji wa mazingira, maendeleo ya jamii ya ikolojia, na elimu ya mazingira. Hivi karibuni Green Zhejiang imeanzisha ushirikiano na NGO yenye makao yake makuu nchini Tanzania ya TEEMO Africa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news