Polisi wadaka matapeli 11 Tanga

TANGA-Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watuhumiwa 11 kwa kujihusisha na utapeli na wizi wa mitandaoni huku wakiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu huo pamoja na fedha za kigeni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, SACP Henry Mwaibambe amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hadija Nyange (35) mkazi wa Wilaya ya Muheza, Zaina Athumani (25) mkazi wa mtaa wa Msambeni jijini Tanga, Omari Mohamedi (27) mkazi wa Mkanyageni jijini Tanga.

Wengine ni Innocent Omeme (35), Abdulazizi Nzori (31), Said Hassan (24), Rashid Habibu (23), Said Juma (30), Iddi Kaniki (35), David Rupiana (22) na Salum Rajabu (24), wote wakazi wa Dar es salaam.

"Watuhumiwa walikamatwa maeneo ya Donge jijini Tanga ambako walipangisha chumba kwa mkataba wa mwezi mmoja kulipa kiasi cha shilingi 800,000.

"Lakini hao pia walikutwa na fedha taslimu shilingi 2,085,300, fedha za Congo shilingi 45,100, pesa ya Marekani dola 1, simu kubwa 11 aina mbalimbali pamoja na simu ndogo za kitochi 13 aina mbalimbali, kadi 42 za simu, katarasi 43 zilizoandikwa namba za simu na majina ya mawakala, lakini pia kadi tano za benki za CRDB, NMB, Posta na Chapchap," amefafanua.

Amesema, baada ya kufanya uhalifu wao walikuwa wakichoma moto laini za simu ambazo wamekwisha zitumia, lakini pia walikutwa na namba za simu mbalimbali 441 ambazo wameziandika kwa ajili ya kutapeliwa.

Kamanda amesisitiza kwamba namba za simu 183 zilitumiwa ujumbe wa kutakiwa kutuma hela na 42 zilikuwa kwenye mchakato ambapo wakishafanya utapeli wanaweka alama ya tiki kwenye namba husika na kwa ambaye yuko kwenye mchakato wanaweka herufi H.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news