Rais Dkt.Mwinyi ateta na ujumbe kutoka Yanga SC na Kaizer Chiefs

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na viongozi wa Timu ya Yanga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,baada ya kumaliza mazungumzo yake na ujumbe huo Julai 23,2023 yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakiwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo, na kutembelea sehemu za Historia ya Zanzibar katika ziara yao ya siku moja ya Kitalii Zanzibar, wakiwa wageni wa Timu ya Yanga African Sport Club.(Picha na Ikulu).
Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati walipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kutembelea sehemu za Utalii Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Rais wa Timu ya Yanga African Sport Club, Mhandisi Hersi Said akizungumza na kuitambulisha Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini walipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kuitambulisha timu hiyo baada ya kumaliza mchezo wao wa Kirafiki wa Tamasha la Wananchi lililofanyika Julai 22, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Da es Salaam. Timu ya Yanga ilishinda mchezo huo kwa bao 1-0.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya jezi ya Yanga ikiwa na jina lake na Rais wa Timu ya Yanga Mhandisi Hersi Said, baada ya kumaliza mazungumzo na Ujumbe wa Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs wakiongozana na viongozi wa Yanga, mazungumzo hayo yalifanyika Julai 23,2023 katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na viongozi na Wachezaji wa Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakiongozana na wenyeji wao Timu ya Yanga African Sports Club, kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar, wakiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja kutembelea maeneo ya Historia ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Timu ya Yanga, Kaizer Chiefs na wachezaji wa timu hiyo baada ya kumaliza mazungumzo yake na ujumbe huo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na viongozi wa Timu ya Yanga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,baada ya kumaliza mazungumzo yake na Ujumbe huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news