Rais Dkt.Mwinyi azihimiza taasisi kuwasilisha michango ZSSF

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi za Serikali na jumuiya zote za waajiri na waajiriwa wahakikishe wanawasilisha michango katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji wa mfuko huo katika kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao wanapostaafu na kuhitaji mafao yao.
Ameyasema hayo leo Julai 25,2023 katika kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kuzindua mradi wa Mji wa Dkt.Hussein Ali Mwinyi uliopo Mombasa Zanzibar pamoja na mfumo wa huduma kwa wateja wa kuwasiliana wa ZSSF WhatsApp ukumbi wa Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt.Mwinyi amewashauri wajasiriamali wote wajisajili na kuchangia Mfuko wa Hiari kupitia mfuko huo, kwani una faida kubwa kwa biashara zao.

Vilevile, amewapongeza ZSSF kwa kuanza kulipa mafao mapya mawili kwa wanachama wake waliopoteza ajira na walioumia wakiwa kazini.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza ZSSF kwa kuzingatia utekelezaji wa agizo lake alilolitoa Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi mwaka huu (2023) kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa wastaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news