Rekodi mpya ya kinubi kilele cha Mlima Kilimanjaro

KILIMANJARO-Hatimaye baada ya safari ya mchana na usiku ya mwanadada mpiga kinubi, kifaa chenye heshima kubwa nchini Ireland, Siobhan Brady leo Julai 25, 2023 ameweka rekodi ya Dunia ya Guiness juu ya Mlima Kilimanjaro, Tanzania.
Siobhan ambaye mwaka 2018 aliweka rekodi Mlima Himalaya, India futi 16,000, sasa leo ameitangaza Tanzania zaidi na Mlima Kilimanjaro kwa kuweka rekodi iitwayo “Guiness World Record for the Highest Harpist Concert” kwenye kilele cha juu zaidi duniani futi 19,000 Uhuru Peak.

Aidha,muda nfupi uliopita alifanikiwa kupiga kinubi kwa dakika 34 ambapo ili kuvunja rekodi alitakiwa walau dakika zisizopungua 18 akichanganya nyimbo mbalimbali kutoka Ireland na mataifa mengine ya Ulaya.

Tukio hilo limerekodiwa na chombo kikubwa cha habari duniani The National Geographic. Sasa Kamati ya Dunia ya Guiness itakaa kuthibitisha rekodi hiyo.

"Ameweza na ameweza tena. Hongera kwa wote waliofanikisha, hongera Watanzania. Hureeeeeee!!!."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news