Rais Dkt.Mwinyi:Serikali inawathamini watoaji msaada wa kisheria nchini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, watoaji msaada wa kisheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa wananchi wasio na uwezo wa fedha kwa msaada wa sheria nchini.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Julai 22, 2023 alipohutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki Msaada wa Sheria mwaka 2023 na utoaji wa Tuzo za Mwaka kitaifa kwa watoa msaada wa kisheria Zanzibar yaliyofanyika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Pia, amesema Serikali itahakikisha marekebisho ya sera na sheria ya msaada wa sheria yanafanyika haraka na kwa ufanisi ili kukidhi matakwa yanayotakiwa kwa utoaji wa msaada wa sheria nchini.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amezipongeza taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kwa juhudi wanazochukua kuwafikia wananchi na kuwafahamisha juu ya upatikanaji wa huduma za sheria nchini.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali itashughulikia kwa haraka masuala yanayowahusu watoaji wa huduma wa msaada wa sheria nchini ikiwemo vitendea kazi vya ofisi na changamoto ya usafiri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news