Rais Dkt.Samia aweka jiwe la msingi ujenzi Mnara na Uwanja wa Mashujaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023. Viongozi wengine pichani ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda wakishuhudia tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka mchanga kama ishara ya uzinduzi wa Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Mkuki na Ngao) kwenye mnara wa Mashujaa katika Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Maafisa pamoja na Wananchi kwenye Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa Heshima ya Wimbo wa Taifa kwenye Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Matukio mbalimbali kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika Katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2023.
Taaswira ya eneo la Uwanja na mnara wa Mashujaa utakavyokuwa katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news