Rekodi ya Dunia kwenda kupiga kinubi kilele cha Mlima Kilimanjaro

KILIMANJARO-Safari ya kuweka rekodi ya Dunia kupiga kinubi juu ya mlima Kilimanjaro (The Highest Harpist Concert) ambayo inaongozwa na dada Siobhan Brady na timu ya watu takribani 92 kwa sasa ipo wastani wa meta 4,000 kuelekea Uhuru Peak meta 5,895 kwenda kutimiza malengo hayo.

Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa vivutio vikubwa zaidi ya utalii ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huu ni mlima ambao umezungukwa na uoto wa asili wa misitu huku ukipambwa na wanyama mbalimnbali wa kuvutia.

Mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi barani Afrika wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).Aidha, pamoja na safu zake tatu za volkeno za Kibo, Mawenzi na Shira ndio mlima mrefu kuliko yote duniani uliosimama peke yake na unaojitegemea.

Huu mlima unaweza kufikika kupitia njia za Rombo, Hai na Moshi ambapo kilele cha Kibo kina urefu wa futi 19,340 (mita 5,895) ambacho ndio killele kirefu katika mlima huo.

Ikumbukwe, Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), ilianzishwa mwaka 1973 pia mlima Kilimanjaro uliteuliwa kuwa eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka 1987.

Historia inaonesha kuwa, mtu wa kwanza wa kufika katika kilele cha mlima huo alikuwa, Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani, Hans Meyer na Ludwig Purtscheller mnamo Oktoba 6, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani.

Safari ya kupanda mlima huo humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za Tropiti hadi Aktiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news