Mkenya amchapa Mandonga

NAIROBI-Pambano la marudiano lililowakutanisha bondia Mtanzania Karim Mandonga (Mtu Kazi) dhidi ya Mkenya Daniel Wanyonyi limemalizika kwa Mandonga kuchapwa.
Pambano hilo la uzani wa Light heavyweight lililoandaliwa katika Kituo cha Maonyesho cha Sarit jijini Nairobi lilifanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Julai 23, 2023.

Licha ya kuwa ugenini, Mandonga bado alikuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao walimshangilia kwa kwa sauti ya juu, wakimtia moyo kumtandika Wanyonyi.

Majaji watatu walimpa Wanyonyi ushindi. Jaji George Athmani alimpa Wanyonyi alama 100-80, Jaji Wycliffe Marende 100-80, na Jaji Leonard Wanga 100-89.

Hili ni Pambano la pili kwa mabondia hao wa Afrika Mashariki kukutana, pambano la kwanza lililofanyika Januari 2023 huko huko Nairobi, Mandonga alimchapa Wanyonyi. (BBC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Miimi ni Mkenya naa tunampenda sana Mandonga. Akiretire boxing anaweza kuwa mtangazaji mzuri sana wa michezo hapa Kenya. Yuko pia na hicho kipawa

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news