Samia Taifa Cup yaungwa mkono

NA SHAMIMU NYAKI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 10, 2023 jijini Dar es Salaam amepokea vifaa vya michezo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Chen Mingjian ambavyo vitatumika katika Programu ya Michezo Mtaa kwa Mtaa pamoja na Samia Taifa Cup.

Vifaa mbavyo Mhe. Chana amepokea ni pamoja na Mipira ya Kikapu 600, mipira ya Wavu 600, mipira ya Miguu 600 pamoja na Jezi 2634.

"Vifaa hivi tutavikabidhi katika mikoa yetu yote Tanzania Bara na Zanzibar bila kusahau Shule zetu mbili za michezo kwa kila Mkoa, naamini vifaa hivi vitanuafaisha vijana wetu katika kukuza vipaji ambavyo vitawasaidia wao binafsi na Taifa letu" amesema Mhe. Chana.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian amesema nchi yake inaendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa wataalamu na ujenzi wa miundombinu ya michezo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news