Serikali yaahidi kuendelea kuimarisha miundombinu ya elimu

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) itajenga vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Muungano iliyopo Halmashauri ya Songea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama na Mbunge wa Peramiho akicheza ngoma za kitamaduni na akinamama wa Kijiji cha Namatuhi wakati wa ziara yake katika Kata ya Ndongosi.

“Tunataka kufanya ukarabati madarasa na kujenga mengine ili Shule ya Msingi Muungano iwe miongoni mwa shule za mfano kwa kuwa na miundo mbinu bora ya elimu;

Mheshimiwa Mhagama ameyabainisha hayo Julai 9, 2023 katika Kijiji cha Namatuhi Kata ya Ndongosi Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vinavyomaliziwa kujengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama na Mbunge wa Peramiho akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Halmashauri ya Songea Vijijini,Thomas Simon Masolwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Muungano.

Waziri Mhagama ameelekeza watendaji wa Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha hatua ya umaliziwaji wa ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa uwe imekamilika ndani kipindi cha wiki mbili.

Akizungumzia kuhusu uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji, Waziri Mhagama amewaomba wananchi wa Kijiji cha Namatuhi kuendelea kuhifadhi mazingira na kuepuka tabia ya ukataji wa miti.

Amesema, chanzo cha maji cha Kitinginyi ndio chanzo pekee kilichobaki, kinapaswa kulindwa ili kuepusha shughuli nyingine za kibinadamu zinazoweza kuharibu chanzo hicho cha maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama na Mbunge wa Jimbo la Peramiho akizungumza jambo na Diwani wa Kata ya Ndongosi, Mhe. Zakaria Mbilinyi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Muungano.

“Tuendelee kutunza chanzo hicho cha maji kwa kupanda miti ili huduma ya maji iweze kunufaisha vijiji vingine vya jirani,"amesema Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Mkugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwalimu Neema Magembe amesema, gharama za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa mpaka ujenzi ulipofikia ni shlingi millioni 34.

Ameongeza kuwa, halmashauri tayari imeshaweka fedha za umaliziaji wa vyumba hivyo madarasa kwa kuweka marumaru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akiweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Muungano iliyopo katika Kijiji cha Namatuhi Kata ya Ndongosi.

Awali Diwani wa Kata ya Ndongosi, Mhe. Zakaria Mbilinyi amemshukuru Waziri Mhagama kwa kutuma Mhandisi wa maji ambaye alifanya utafiti na kugundua chanzo cha maji katika Kitongoji cha Muungano kilichopo katika Kijiji cha Namatuhi Kata ya Ndongosi.

“Wananchi wana matumaini makubwa, kwamba watapata huduma ya maji safi na salama,” alisema Mhe. Mbilinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news