Serikali yakamilisha maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani

NA ELEUTERI MANGI-WUSM

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita amesema, maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo mwaka huu kitaifa yanafanyika jijini Zanzibar Julai 7, 2023 yamekamilika na yatakuwa na shamrashamra mbalimbali ikiwemo muziki wa taarab kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Lengo la kuadhimisha Siku ya Kiswahili ni kuieleza Dunia kuwa chimbuko la Kiswahili ni Tanzania.
Mhe. Waziri Tabia amesema hayo Julai 3, mjini Zanzibar wakati wa mkutano wa na waandishi wa Habari mjini humo kutambulisha maadhimisho ya pili ya Siku ya Kiswahili ambayo yalianza kuadhimishwa mwaka 2022 baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu amesema tamasha hilo litahudhuriwa na watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Ujerumani, Ghana, Kenya, Visiwa vya Comoro na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news