Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) layakutanisha mataifa 20

NA ELEUTERI MANGI-WUSM

TAMASHA la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limehitimishwa ambapo nchi zaidi ya 20 zimeshiriki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Cameroon, Qatar, Congo DRC, Misri, Algeria, Tunisia, Morocco, Italy, Israel, Ufaransa, Uingereza, Ireland, Afghanistan, Denmark, Hispania, Angola, Namibia, Afrika Kusini, China, Zambia, Zimbabwe na Uswisi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akikabidhi tuzo ya filamu kwa mmoja wa washindi wa tuzo hizo wa Tanzania wakati wa kufunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 2, 2023 mjini Zanzibar.

Tamasha hilo limehitimishwa Julai 2, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma ambaye alitoa tuzo kwa filamu bora na ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) ya EONII iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam 
Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Dkt. Kilonzo Kiagho ni miongoni mwa wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani kutoka mataifa hayo. 

Ni mwaka wa 26 tangu Tamasha la ZIFF lilipoanzishwa mwaka wa 1997 kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na mambo mengine ya kiutamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa kikanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news