Sijaridhika na kasi ya ujenzi-Dkt.Msonde

IRINGA-Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Dkt. Charles Msonde amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule mpya na madarasa ya shule za msingi na awali kupitia mradi wa BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Dkt. Msonde amesema hayo wakati akikagua ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa baada ya kujionea ujenzi ukiwa hatua za awali katika baadhi ya shule.

Dkt. Msonde amebaini ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo Halmashauri iliamua kufanya manunuzi kwa kuagiza vifaa viwandani kwa pamoja moja ili kubana matumizi na kupelekea ujenzi kuchelewa kuanza kwa miezi mitatu.

Dkt. Msonde amemuagiza Katibu Tawala Mkoa Iringa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi huo wa BOOST Ili kubaini waliokiuka miongozo na tararibu utekelezaji mradi huo zilizotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI

“katibu Tawala fanya uchunguzi ili tujue nani alikwenda kinyume na maelekezo na miongozo ya Serikali katika kufanya manunuzi na kusababisha ujenzi kutoanza kwa wakati,” Dkt. Msonde amesisitiza.

Aidha, Ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Iringa kuhakikisha wanaongeza nguvu kazi mafundi ili kuhakikisha miundombinu yote inakamilika na kuanza kutoa huduma.

Dkt. Msonde amesema, Serikali haitomvulia mtu yeyote anayekwamisha juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa ajili ya manufaa ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news