Simba SC wafika ubalozini Uturuki

ANKARA-Kikosi cha Simba SC kimetembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki na kuzungumza mambo mbalimbali na mwenyeji wao, Balozi Luteni JeneraliYakubu Hassan Mohamed.

Luteni Jenerali Yakubu aliwatakia maandalizi mema kuelekea mashindano yaliyo mbele yao huku akiwakumbusha wachezaji kuhakikisha wanapambana uwanjani kusaidia timu kupata ushindi.

“Nimefurahi sana kukutana nanyi hapa, nawakaribisha sana Uturuki jisikieni mpo nyumbani, sisi tutahakikisha mnapata kila kitu ambacho mnastahili.

“Binafsi niwatakie maandalizi mema kuelekea msimu mpya wa mashindano, kikubwa nasisitiza kwa wachezaji mjitume uwanjani kuipa timu ushindi na kuwapa furaha mashabiki,”amesema Balozi Yakubu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news