Simba SC,Zira FC zatoka sare mchezo wa kirafiki

ANKARA-Mchezo wa kirafiki kati ya Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam na Zira FC ‘The Eagles’ katika Uwanja wa Vonresort nchini Uturuki umemalizika kwa suluhu ya bao 1-1.

Simba SC imevaana na Zira FC ambayo ni timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbaijan ambapo mchezo huo wa Julai 24,2023 ulianza kwa kasi katika dakika 15 za kwanza huku timu zote zikishambuliana kwa zamu, lakini hakuna iliyopata bao.

Dakika ya 19 Zira FC walipata penati baada ya mchezaji wao kufanyiwa madhambi ndani ya 18, lakini mkwaju huo uliopigwa na Filip Pahtmann uliokolewa na mlinda mlango Ally Salim.

Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 33 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Said Ntibazonkiza.

Baada ya bao hilo Zira FC waliliandama lango la SC na kufanya mashambulizi kadhaa, lakini ukuta wa Simba SC ulionekana kuwa imara.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikiwa na dhamira ya kutafuta bao, lakini umakini wa kutumia nafasi zilizopatikana ulipungua.

Zira FC walipata bao la kusawazisha kupitia Rustam Ahmadzade dakika ya 63 baada ya kuunganisha krosi ya Fuad Bayramov.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ alifanya mabadiliko ya kuwatoa Willy Onana, Aubin Kramo, na Sadio Kanoute na kuwaingiza Clatous Chama, John Bocco, Fabrice Ngoma na Israel Patrick.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news