TARURA waanza ujenzi wa Daraja la Mto Njoka

RUVUMA-Serikali imetoa shilingi millioni 699 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mto Njoka lenye ukubwa wa mita 20 na ambalo litapitika muda wote na kusaidia kufungua barabara ya Muhukuru mpaka Kizuka itakayochochea uchumi kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akiwa na Mhandisi Johson Kweka wa TARURA katika eneo la ujenzi wa Daraja Mto Njoka wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Songea.

Kauli hiyo Julai 13, 2023 imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katka Halmashauri ya Wilaya ya Songea. 

“Barabara hii ni barabara muhimu, ni barabara ya huduma ni barabara ya uchumi ni barabara itakayoimarisha ulinzi,na kipekee ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja,"amesema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amefafanua, serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga daraja la mto Mgugusi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili madaraja yote makubwa yaweze kupitika katika majira yote ya mwaka wakati wa mvua na wakati wa kiangazi.

Aidha, ujenzi wa madaraja madogo madogo manne umekamilika na wakala wa barabara vijijini TARURA wanamalizia ujenzi wa madaraja mengine manne madogo madogo yaliyobakia katika ujenzi wa barabara.

“Ukamilishwaji wa ujenzi wa barabara utarahisishia wananchi kupata huduma ya usafiri kwa haraka na kuchochea ukuaji wa miji,”amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mhe. Menas Komba amesema, ujenzi wa daraja hilo utasaidia serikali kuongeza mapato katika mazao ya bishara na chakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Njoka.

“Barabara inaenda kuwakomboa wakulima wa wilaya ya Songea kwa kurahisisha huduma ya usafiri, na tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi kwa kusimamia vizuri ilani,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Songea Vijijini, Thomas Masolwa amempongeza Mhe. Rais kwa kutatua changamoto kwa wananchi, na kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka.
Awali katika taarifa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Johson Kweka alisema, Mkandarasi HERA Construction ameshatekeleza kazi za kusafisha eneo la daraja, kuondoa miti katika eneo la mradi, kuchimba udongo na kupasua mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa daraja.

Amefafanua kwamba, Mkandarasi anaendelea na ufungaji wa nondo na boksi kwa ajili ya ufungaji wa nguzo na mikono ya daraja na ujenzi umefika asilimia 40.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news