Ummy Nderiananga azidi kuwaunganisha wanawake

NA MATHIAS CANAL
Kilimanjaro

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mheshimiwa Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) amenunua kadi 3,500 kwa kwa ajili ya wanachama wapya wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro ili kuimarisha chama hicho katika ngazi ya wanawake.

Akizungumza Julai 21,2023 mbele ya Vikundi vya Wanawake Wilaya ya Moshi Vijijini katika ofisi za CCM wilayani hapo amesema kuwa, amechukua hatua hiyo baada ya maombi ya akina mama waliyoyatoa wakati wa ziara zilizofanywa na viongozi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro

“Niwapongeze viongozi mbalimbali wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ziara mlizozifanya, lakini katika ziara zile nimeskia wakinamama wakisema wanahitaji kadi za UWT, kwa hiyo nikapokea ombi hilo na leo nimelifanyia kazi nimeleta kadi,”amesema.

Amesema kuwa, amenunua kadi 3500 kwa ajili ya wanachama wapya wa Umoja wa Wanawake wa chama cha hicho na anategemea kila wilaya katika mkoa huo itapata kadi 500.

Pia, Mheshimiwa Ummy Nderiananga ameunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuviwezesha vikundi vya wanawake kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa mitungi ya gesi huku akisisitiza umuhimu wa nishati hiyo mbadala.

Amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan imelenga kuhakikisha inapunguza matumizi ya kuni, mkaa na mabaki ya mazao ili kulinda afya za wananchi.

Mheshimiwa Nderiananga amesema kuwa, licha ya athari za kimazingira zinazotokana na ukataji wa miti unaofanywa na wananchi kwa ajili ya matumizi ya nishati chafu yamekuwa na athari zaidi za kiafya kama takwimu za athari ya matumizi hayo zilivyotolewa na Wizara ya Nishati hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news