Waache kuuza viungo vya mwili

RUVUMA-Vijana nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuuza viungo vyao vya mwili ikiwemo figo ili kuepukana na madhara ya kiafya.

Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Mpango akiwa ziarani mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua jengo la kutolea huduma ya usafishaji figo lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph Peramiho.

Mheshimiwa Dkt.Mpango amesema, utoaji wa figo unaweza kuhatarisha maisha hususani figo iliyobaki inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Pia, amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kuepukana na hatari za maradhi mbalimbali na kufikia hatua mbaya zaidi.

Wakati huo huo ameshauri kuachana na ulaji usiofaa, unywaji wa pombe kupitiliza pamoja na kuhimiza kufanya mazoezi kuepukana na hali hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia Julai 20,2023 hadi Julai 24,2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news