Washuhudia maboresho makubwa huduma za afya Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Abdalla Shaibu Kaim na timu yake wameipongeza Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa michango mikubwa ya kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Musoma Vijijini mkoani Mara.
Vilevile, wananchi na viongozi wao wa Chama na Serikali wa Musoma Vijijini wamepongezwa kwa kazi nzuri wazifanyazo kwenye utekelezaji ya miradi ya maendeleo ya vijiji vyao.

Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya kata 21 zenye Vijiji 68 na vitongoji 374. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Julai 11, 2023 chini ya Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo wanavijiji na viongozi wao mbalimbali wanaendelea kushirikiana na Serikali kujenga na kuboresha miundombinu ya utoaji wa Huduma za Afya kwenye maeneo yao ya vijijini, kama ifuatavyo:

Hospitali ya hadhi ya wilaya moja inaendelea kujengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero katika Kijiji cha Suguti. Huduma ndogo ndogo (OPD) zimeanza kutolewa hapo.

Pia, kati ya vituo vya afya sita, vinavyotoa huduma za afya ni vitatu ikiwemo cha Murangi, Mugango na Bugwema.

Vituo vipya vya afya vinavyosubiri kupewa wafanyakazi na vifaa tiba ni vitatu kikiwemo Makojo, Kiriba na Kisiwani Rukuba (inatoa huduma kwa hadhi ya zahanati).

Aidha, kati ya zahanati 41 zinazotoa Huduma za Afya ni 24 ikiwemo ya Bugoji, Bugunda, Bukima, Busungu, Bwai Kwitururu, Chitare, Etaro, Kiemba, Kigera Etuma, Kiriba, Kome, Kurugee, Kwikuba, Masinono, Mayani, Mmahare, Mwiringo, Nyakatende, Nyambono, Nyegina, Rusoli, Seka, Suguti na Wanyere.

Zahanati Binafsi zinatoa Huduma za Afya ni nne ikiwemo Bwasi (SDA), Mji wa Huruma (Katoliki), Kwibara (KMT) na Rwanga (KMT).

Wakati huo huo, zahanati mpya zinazojengwa ni 13 ikiwemo Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kurukerege, Kurwaki, Maneke, Mkirira, Nyambono na Nyasaungu.

Kwa upande wa magari ya kusafirisha wagonjwa (Ambulances),Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameleta na kugawa magari matano ya wagonjwa kama ifuatavyo:

Kituo cha Afya cha Murangi (ambulance kubwa ya kisasa), Zahanati za vijiji vya Masinono (sasa Kituo cha Afya cha Bugwema), Kurugee, Nyakatende na Mugango (sasa Kituo cha Afya cha Mugango).

Mbali na hayo, Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Kurwaki Julai 10,2023 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaibu Kaim aliweka jiwe la msingi kwenye Zahanati ya Kijiji cha Kurwaki iliyoanza kujengwa na wananchi wa kijiji hicho wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo, Madiwani na Viongozi wao wengine.

Serikali imeanza kuchangia kwa kutoa shilingi milioni 50 kwenye ujenzi wa zahanati hiyo.Mkuu wa Wilaya (DC), Dkt. Khalifan Haule na Mwenyekiti wa CCM Wilaya,Denis Ekwabi na timu zao, wamepongezwa kwa kusimamia na kuratibu mbio za Mwenge Jimbo la Musoma Vijijini kwa mafanikio makubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news