Watu 10 kutoka Afrika Kusini wawasili nchini kujifunza ufugaji nyuki

DODOMA-Serikali ya Tanzania imepokea ugeni wa watu 10 kutoka nchini Afrika Kusini waliofika nchini kwa lengo la kujifunza juu ya ufugaji nyuki hasa kwenye uanzishwaji wa Manzuki na Hifadhi za nyuki, maandalizi na ukaguzi wa Manzuki pamoja na kuzuia na kudhibiti wadudu kwenye ufugaji nyuki.
Akiongea leo mara baada ya Wageni hao kuwasili, Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba amesema ziara hiyo ni ya kimkakati katika kuanzisha mazungumzo na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini hususan katika eneo la biashara ya mazao ya nyuki, teknolojia za ufugaji nyuki na utafiti.Amefafanua kuwa ugeni huo wa Watu 10 unajumuisha Wataalam pamoja na wafugaji nyuki. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Deusdedith Bwoyo amesema wageni hao kutoka nchini Afrika Kusini wamehamasika kuja hapa nchini kujifunza namna shughuli za ufugaji nyuki zinavyofanyika.
“Kule Afrika Kusini tumeambiwa wana uwezo wa kuzalisha tani 2000 kwa mwaka wakati asali inayohitajika ni tani 4000 kwa mwaka, Sisi huku tuzalisha tani 32,691 kwa mwaka na tunatumia asali hiyo ndani ya nchi karibia asilimia 90,” amesema Bwoyo.
"Wamekuja kujifunza ni kwa namna gani tunaweza kuongeza uzalishaji wa asali kule kwao, na pili namna gani wanaweza kuwahamasisha watu kule kwao kutumia asali kama ambavyo sisi tunafanya hii ndio sababu kuu ya ujio wao."

Naye, Kiongozi wa Wajumbe hao ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Maendeleo Vijijini Kaskazini Magharibi mwa Afrika Kusini, Zakaria Thupi Mokgathlha, amesema Tanzania ni nchi ambayo imepiga hatua kubwa kwenye eneo la ufugaji nyuki, hivyo wamekuja kujifunza ili waweze kupata ujuzi utakao wasaidia kujiimarisha kwenye neo hilo.
“Tumekuja kuangalia Tanzania inavyofanya kwenye eneo hili ili tutakavyorudi kwetu tukaweke mikakati ya kuimarisha sekta hii,” amesema Zakaria. 
Katika ziara hiyo, Wataalamu hao watatembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki kilichopo mkoani Tabora uongozi wa mkoa huo pamoja na vikundi vya wafuga nyuki vya mkoa huo.
Vilevile, mara baada ya kuwasili Dodoma wametembelea Ofisi za Manyoni za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) pamoja na Hifadhi ya Nyuki ya Agondi ambapo wamepata elimu ya namna bora ya kufuga na kuchakata mazao ya nyuki hususani Asali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news