Serikali yaridhishwa na uzalishaji mbolea ITRACOM Dodoma

DODOMA-Waziri wa Viwanda na Biashara,Mheshimiwa Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amesema, Serikali itaenda hatua kwa hatua kuhakikisha changamoto wanazopata wenye viwanda zinatatuliwa na kushughulikiwa kwa wakati.
Dkt.Kijaji amesema hayo leo Julai 26,2023 alipotembelea Kiwanda cha Mbolea ITRACOM kilichopo Nala jijini Dodoma kujionea uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho.
Aidha, amekipongeza kiwanda hicho kwa utengenezaji wa mbolea usiokua na mchanganyiko wa asilimia 100 ya madini, bali asilimia 50 ni samadi na asilimia 50 ni madini ambao unaleta uhai wa ardhi kwa uasili na ubora wake 
Amesema, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho kwa awamu ya kwanza, kitaweza kuzalisha tani millioni 1.2 kwa mwaka huku matumizi ya ndanj ya nchi ni tani 650,000 hivyo hakuna sababu ya kuagiza mbolea nje ya nchi. 
Dkt.Kijaji amesema, amezikaribisha nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ikiwemo Kenya ambayo tayari imeshanunua tani 3000 za mbolea kununua mbolea kutoka ITRACOM kutoka Dodoma Tanzania.
Naye Mkurugenzi wa ITRACOM ,Bw.Nduwimana Nazaire ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutambua juhudi za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho na ameiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kushirikiana na wizara zingine katika juhudi za usambazaji wa mbolea hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news