Waziri Mhagama atembelea Mnara wa Shujaa UD 5826 L/CPL Ahamad Mzee

MTWARA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ametembelea Mnara wa Shujaa UD 5826 L/CPL AHAMAD MZEE katika Kata ya Kitaya Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mkuu, Kanali Ahmed Abbas akitoa heshima mbele ya Mnara wa Shujaa UD 5826 L/CPL AHAMAD MZEE katika Kata ya Kitaya Halmashauri ya wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara.
Waziri ametembelea mnara huo Julai 17,2023 Nanyamba mkoani Mtwara siku chache kuelekea Siku ya Mashujaa ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika Agosti 28,2023 katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 

Shujaa Ahmad Mzee alikuwa mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kikazi akiwa na umri wa miaka 21 alipelekwa mpakani mwa Kijiji cha Kitaya akiwa na jukumu la Ulinzi wa Taifa la Tanzania katika nafasi ya mpiga mzinga wa kuangusha ndege.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas katika eneo la Mnara wa Shujaa UD 5826 L/CPL AHAMAD MZEE katika Kata ya Kitaya Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara.

Katika kutekeleza majukumu yake tarehe 14 Aprili 1972 wakati ndege za Mreno zikitokea Msumbiji Helicopta na Jet Fighters zilipiga mabomu Kijiji cha Kitaya na katika Mapambano hayo Shujaa Ahmad Mzee aliangusha Jet Fighter mbili, moja ilianguka ardhi ya Tanzania Mto Ruvuma na nyingine ilianguka ardhi ya Msumbiji.

Kwenye mapambano hayo Shujaa Ahamad Mzee alijeruhiwa baada ya kupigwa na fighter na alichukuliwa na kukimbizwa Mtwara Ligula Hospitali na huko ndiko alikofia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news