Waziri Ummy:Wataalam wa afya wa mikataba waajiriwe

SHINYANGA-Waziri wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameagiza halmashauri zote nchini kuajiri wataalamu wa afya wa mikataba ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma bora na haraka kwa Watanzania.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Julai 13, 2023 alipokuwa anaongea na Timu ya Usimamizi wa Afya ya Mkoa pamoja na Wataalamu wa Afya ngazi ya Jamii kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake mkoani humo.

“Naagiza halmashauri zote nchini kuajiri wataalam wa afya wa mikataba ili tuendelee kutoa huduma bora kwa Watanzania na kwa haraka,"amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ametaka huduma bora za uangalizi kwa watoto wachanga (NICU) ziwepo katika hospitali za halmashauri zote nchini ili tuokoe maisha ya watoto.

“Maelekezo yangu nataka kila kila Hospitali ya Halmashauri zitoe huduma za uangalizi kwa watoto wachanga (NICU) sababu tunataka kila mzazi anaekwenda kujifungua katika Hospitali atoke na mtoto wake,”ameongeza Waziri Ummy.

Pia,Waziri Ummy amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafanya jukumu lake la kutoa fedha katika Sekta ya Afya na Sasa ni jukumu la Wataalam wa Afya kutoa huduma bora kwa Watanzania.

“Tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali Afya za Watanzania ametoa fedha za majengo, ametoa fedha za vifaa na vifaa tiba, fedha za dawa sasa ni jukumu letu sisi watendaji kutoa huduma bora kwa Watanzania,”amesema Waziri Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news