Rais Dkt.Samia aomboleza kifo cha Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameelezea kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam, Hemedi Bakari Mkali.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameyabainisha hayo leo Julai 13, 2023 kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mzee Hemedi Bakari Mkali, Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam.

"Pole kwa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Tangu harakati za kudai uhuru na hata sasa, kujitoa kwa hali na mali, na busara za wazee wa Dar es Salaam na kwingine kote nchini kumekuwa sehemu muhimu ya ushauri na mwanga katika mambo yenye kuleta tija kwa nchi yetu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina,"amebainisha Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news