Waziri wa Fedha ateta na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) Kanda ya Afrika

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Floribert Ngaruko, baada ya Mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mhe. WF, Ofisi ya Hazina Ndogo, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha pia Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, Naibu Katibu Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Floribert Ngaruko, akizungumza jambo wakati wa Mkutano na ujumbe wa Tanzania, uliongozwa na Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayumo pichani), uliofanyika Ofisi ya Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi huyo, Bw. Venuste Ndikumwenayo.
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Floribert Ngaruko (wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali,, Dkt. Natu El-maanry Mwamba (wa pili kushoto), Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (kushoto), na Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Bw. Venuste Ndikumwenayo (wa kwanza kulia), baada ya Mkutano wao kuhusu ushirikiano wa Serikali na Benki hiyo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mhe. WF, Ofisi ya Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF-Dar es Salaam).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news