WHO yaunga mkono tafiti magonjwa yasiyoambukiza

DODOMA-Shirika la Afya Duniani (WHO) inatarajia kuipatia Tanzania shilingi milioni 855 kwa ajili ya kuwezesha kufanya utafiti wa kitaifa wa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza (Steps Survey 2023) unaotarajiwa kuanza mapema Agosti, mwaka huu nchi nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Nassor Mazrui jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof.Said Abood amesema, fedha hizo zitazaidia kukamilisha zoezi hilo kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Prof.Abood amesema kuwa, Utafiti wa “Steps Survey” ni ufuatiliaji wa viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza ili kukusanya takwimu muhimu kuhusu Magonjwa yasiyoambukiza na viashiria vya hatari vya magonjwa hayo.

“Tafiti hii itatoa taarifa muhimu kuhusu hali ya afya na jamii yetu na kutambua matendo ya maboresho katika afya na kuweka mikakati kwa ajili ya kuboresha Matendo hayo kwa lengo la kuimarisha afya ya Jamii yetu,”alisema Prof. Abood.

Alisema, takwimu ndio kiini cha kujenga Taifa lenye afya bora. “Takwimu tutakazokusanya kupitia Utafiti huu zitatumika kama dira ya kutuongoza kuelekea kutengeneza mikakati yenye ushahidi ili kuboresha afya za watanzania.

Vile vile alisema takwimu zitawafanya kuelewa viashiria vya hatari vya magonjwa yasiyoambukiza kama vile ulaji usiofaa, kutokufanya mazoezi ya mwili na unywaji wa pombe kupita kiasi na kunaweza kubuni mbinu zitakazoshughulikia visababishi hivyo vikuu vya NCDs.

Naye, Mwakilishi wa WHO Dkt. Alphoncina Nanai alisema Magonjwa Yasiyoambukiza yameanza kuwa tatizo kubwa ulimwenguni.

Alisema, katika kila vifo 10, vifo 7 vinasababishwa na magonjwa Yasiyoambukiza ulimwenguni na watu milioni 17 wanafariki ambapo 86% ya vifo vinatoka nchi za Afrika.

Aidha, Dkt. Nanai alisema Magonjwa Yasiyoambukiza yanaweza kuzuilika ndio WHO na Serikali ilianzisha utaratibu wa kupima miaka kumi iliyopita ili kujua uzito wa magonjwa hayo na yanakuaje.Alisema wanafuatilia magonjwa hayo kwani wapo watu wengi hawajui kama wana magonjwa hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news