Dawa za kulevya zakamatwa Arusha

ARUSHA-Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuanzia Julai Mosi, 2023 hadi sasa kupitia operesheni mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya limefanikiwa kukamata mirungi kilogramu 257.3, bangi kilogramu 98 pamoja na heroine gramu 100.

Akitoa taarifa hiyo Agosti 18, 2023 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amesema, mbali na dawa hizo pia wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 32 wakiwa na pombe ya moshi lita 238.5 pamoja na mitambo minne ya kutengeneza pombe hiyo.

ACP Masejo amesema, pia wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 28 wa makosa ya ukatili na baadhi yao wamehukumiwa kwenda jela vifungo mbalimbali.

Kati ya waliohukumiwa, watuhumiwa watatu walihukumiwa kwenda jela vifungo vya maisha kwa makosa ya ubakaji na ulawiti na mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji.

Kamanda Masejo amesema, mafanikio hayo yametokana na elimu ambayo inaendelea kutolewa kwa wananchi ambao wamekua wakitoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kupelekea mkoa huo kuendelea kuwa shwari hasa kwa kuzingatia ni kitovu cha utalii nchini.

Pia,ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Kamanda huyo amewataka watu wachache wanaojihusisha na uhalifu kuacha mara moja vitendo hivyo, kwani jeshi hilo halitasita kuwakamata na kuchukua hatua za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news