DC Mkasaba atoa wito kwa wadau wa kilimo

NA FAUZIA MUSSA 

MKUU wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mhe.Rajab Mkasaba amewataka wadau wa kilimo kutumia vyema fursa ya elimu walioipata katika maonesho ya wakulima (Nane name) ili kuleta mageuzi ya kilimo nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mhe. Rajab Mkasaba akipata maelezo kuhusiana na NTA kutoka kwa mfugaji Nyuki wakati alipotembelea maonesho ya ya kilimo yaliyofanyika Dole Wilaya ya Magharibi A. (PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANIZIBAR).

Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo yaliyofungwa Agosti 10 huko Dole Wilaya ya Magharibi A amesema maonesho hayo hayakuwa kwa ajili ya kujionea bidhaa za kilimo tu,Bali pia yalijikita katika kuwapatia wananchi elimu kuhusiana na kilimo.Hivyo aliwataka wadau hao kufuata malekezo ya wataalamu ili kuhakiksha wanalima ,kufuga na kufanya shughuli za Uvuvi wa kisasa.

Aidha Mhe. Mkasaba alipongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya kilimo kwa kuboresha maonesho hayo yanayotoa fursa Kwa wakulima ,wajasiriamali na wadau wa kilomo kuweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusuiana na mambo mbalimbali ya Kada hiyo.

Vile vile aliwashauri wadau hao kuwa Mabalozi wazuri kwa wenzao kwa kuweza kuwapatia elimu,uzowefu na ujuzi walioupata katika maonesho hayo ili kurithisha kilimo bora kizazi hadi kizazi

“kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa wataalamu wametuelekeza kulima kisayansi ,shamba dogo mazao mengi na yenye bora ni wakati wakubadilika sasa ”alisisistiza Mkuu huyo

Awali Mkuu wa Wilaya alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuzindua maonesho hayo mwanzoni mwa mwezi huu sambamba na kukubali ombi la Wizara ya kilimo la uboreshaji wa miundombinu ya Barabara katika eneo Hilo Jambo ambalo litawarahisishia wananchi kufika katika maonesho hayo kwa urahisi.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe Rajab Mkasaba akipata maelezo kuhusiana gesi asilia ambayo hutengenezwa kwa kutumia kinyesi cha Ng'ombe kutoka kwa Luteni Kanali wa JKU Ramadhan Ali Hassan alipotembelea maonesho ya wakulima yaliyofanyikaWilaya ya Magharibi A.

Hata hivyo, Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuishauri Wizara ya Utalii na Mambo yakale kwa kushirikana na Wizara ya kilimo kuhakikisha wanayatangaza zaidi maonesho hayo kwa wageni wanaotoka Nchi mbali mbali kuja Kutalii Zanzibar katika Msimu wa Maonesho ili wawe daraja la kuitangaza Zanzibar kupitia bidhaa adimu zinazotokana na kilimo Visiwani humu.

"Zanibar tuna matunda adim ambayo wenzetu hawana kama shoki shoki doriani nashauri tuwashajihishe watalii kuja kujionea bidhaa hizo ili na wao waweze kuzitangaza nchi kwao"

Baadhi ya wadau wa kilomo waliojitokeza katika maonesho hayo walisema maonesha yamewasaidia kupata elimu na kubadilishana uzowefu Kati ya wajasiriamali,wakulima,wafigaji na wavuvi

Hivyo wameahidi kuifanyia kazi elimu hiyo na uzowefu walioupata katika maonesho hayo ili kuleta mabadiliko ya kilimo nchini.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wakulima Duniani hufanyika kila ifikapo agosti 8 ya kila mwaka ambapo kitaifa maadhimisho hayo yalifanyika Jijini Mbeya yakiwa na kauli mbiu “VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA KWA MIFUGO ENDELEVU YA CHAKULA.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news