Dkt.Biteko amshukuru Rais Dkt.Samia

NA MATHIAS CANAL

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kutoa fesha kiasi cha shilingi 300,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe.
Mradi huo unatarajiwa kutoa huduma za dharura kwa jamii na wasafiri wanao tumia barabara kuu inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi huku kiasi cha wananchi wapatao 100,051 watahudumiwa.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini,Dkt.Doto Biteko ameyasema hayo leo tarehe 6 Agosti 2023 mjini Bukombe wakati akizungumza na wananchi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua jengo la ICU Wilaya ya Bukombe. 
"Nafurahi kusema kwamba serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha watu mahututi (ICU) ili tuache kuwapeleka watu wetu mbali kwa ajili ya huduma hiyo badala yake waipate hapa hapa.

"Ndugu kiongozi wa mbio za mwenge Tufikishie salamu zetu kwa Rais, mwambie mama kwenye kazi uliyoifanya Bukombe katika kila sekta watu wale wamekuandalia maua yako."
Dkt.Biteko amesema kuwa, Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi huku akimshukuru pia kwa kutenga fedha kwa ajili ya Ujenzi wa chuo cha VETA Bukombe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news