Hakuna kinachosimama, Ushetu wamshukuru Rais Dkt.Samia

NA MATHIAS CANAL

MBUNGE wa Jimbo la Ushetu lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Dkt Emmanuel Cherehani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati.
Amesema kuwa, Rais Dkt.Samia amekuwa kinara kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ambapo ametaja mafanikio ya miradi mbalimbali ikiwemo kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani ambapo upatikanaji wa maji safi na salama katika Jimbo la Ushetu umeongezeka.

Dkt.Cherehani ametoa pongezi hizo katika Kijiji cha Ulewe wakati akizungumza na wananchi kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema kuwa, kwa mafanikio ya miradi mbalimbali Rais Samia anaenda kuandika historia kubwa katika Jimbo la Ushetu na nchi kwa ujumla wake.

Amesema kuwa, Jimbo la Ushetu katika uongozi wa Rais Samia imepokea shilingi bilioni 6.1 kwa ajili ya miradi sita ya maji ikiwemo mradi wa Sabasabini-Mpunze, Igwamanoni, Nyankende, na mradi wa maji wa Nyamilangano.
Kadhalika katika sekta ya elimu amesema kuwa, Jimbo la ushetu limepokea shilingi 2.89 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 108 ya sekondari ambayo wananchi hawajachangishwa kiasi chochote.

Amezitaja shule hizo ambazo ni pamoja na Eliasi Kuandikwa iliyojengwa kwa shilingi 470, Shule ya Sekondari Cherehani iliyoko Ubagwe ambayo imejengwa kwa shilingi 300, na zaidi ya shilingi bilioni 1.88 za mradi wa BOOST kwa ajili ya shule za msingi Nyankende na Ukune na nyumba ya mwalimu pamoja na nyumba ya mkurugenzi.
Kuhusu miundombinu ya barabara Mbunge Cherehani amesema kuwa, serikali inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kuimarisha miundombinu ambapo katika kipindi cha muda mfupi barabara nyingi zinapitika ipasavyo.
Amesema kuwa Wilaya ya Ushetu imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Rais Samia anapata kura za kutosha wakati wa uchaguzi mkuu wa 2025 kutokana na amendeleo anayoyafanya katika kipindi cha muda mfupi tangu aingie madarakani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news