Hongereni kwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano nchini.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo alipokutana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha baada ya kuchaguliwa mwezi Februari mwaka huu kuliongoza Kanisa hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru viongozi wa kanisa hilo kwa mipango yao ya kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii na Serikali ipo tayari kuendeleza ushirikiano na kanisa katika sekta hiyo.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar. Vilevile Askofu Mndolwa amesema, kanisa linaendelea kumuombea katika uongozi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news