Waguswa na ufanisi bora wa Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema ataendelea kujitahidi kutimiza ahadi alizowaahidi wananchi wa Zanzibar na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo alipokutana na Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar waliofika Ikulu Zanzibar leo Agosti 30, 2023.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mialiko ya wenyeviti hao kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi mwaka huu.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Mzee Hassan Wakasuvi akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa CCM wa mikoa amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa mabadiliko ya maendeleo yaliyofanyika Zanzibar chini ya uongozi wake.

Sambamba na kuendelea kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa kutimiza ahadi na kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar pia amempa moyo kuwa viongozi walioko Tanzania Bara kuwa wamejionea mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news