Kongamano la Saba la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi kufanyika mwezi ujao Dodoma

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la saba la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ambalo linaratajiwa kufanyika Septemba 29,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma wa Baraza, Bw. Gwakisa Bapala (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Uwezashaji na Ushiriki wa watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati, Bw.Silaji Nalikame muda mfupi baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi litakalofanyika septemba 29, mwezi ujao jijini hapa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa amewaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa, kongamano hilo umuhimu litatanguliwa na wiki ya uwezeshaji sambamba na maonesho ya siku tatu ya wajasiriamali yatakayoanza Septemba 26 hadi 28 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

“Maenesho hayo ya siku tatu kabla ya kongamano yana maana kubwa katika dhana nzima ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwani wajasiriamali watapata fursa ya kipekee kuonyesha biashara zao kwa watanzania na jinsi wanavyopata mafanikio kupitia uwezeshaji,” alisema Bi. Issa.

Kwa mujibu wa Katibu huyo Mtendaji wa Baraza, Kauli Mbiu ya Kongamano hilo la saba ni ‘Uwezeshaji kwa Uchumi Endelevu’ kwani inatoa fursa ya kujadili kwa kina masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa uchumi endelevu wa Tanzania.

“Kongamano litatoa pia fursa ya kutathmini utekelezaji wa sera ya uwezeshaji pamoja na taarifa mbalimbali ya utekelezaji wa mambo yaliyokuwa kwenye kongamano la sita ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaagiza wakuu wa mikoa yote kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi,” alisema.

Bi.Issa alisema wakati wa kongamano, tuzo pia zitatolewa kwa wote waliofanya vizuri ikiwemo mkoa uliofanya vizuri, wajasiriamali na taasisi mbalimbali za uwezeshaji kwani mafanikio mengi yameshapatikana chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

“Kama Baraza tunamshuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na ufuatiliaji wake wa kutaka kuona kuwa watanzania wengi na hasa wanawake na vijana wananufaika zaidi na uwezeshaji sambamba kuinua vipato vyao na kuchangia pato la taifa,” alisema.

Alisema kongamano litahusisha Wizara, Mashirika, Wakala na Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Mikoa, Halmashauri, Wajasiriamali, Taasisi za Fedha, Taasisi za Elimu, Tafiti, Wawekezaji pamoja na wadau wengine wa masuala ya uwezeshaji.

“Wananchi wote wanakaribishwa wanakaribishwa kujionea na kujifunza masuala mazima ya uwezeshaji, upatikanaji wa mitaji, fursa zilizopo kwenye miradi ya mkakati,masoko na hata kutengeneza mtandao wa watu, Taasisi au Kampuni ya kujiendeleza kiuchumi,” alisisitiza Bi. Issa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news