Mahafali ya 15 Furahika Education College yafana

DAR ES SALAAM-Chuo cha Maendeleo ya Ujuzi, Ufundi na Viwanda (Furahika Education College) kilichopo Buguruni Malapa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam kimefanya mahafali ya 15.
Mahafali hayo yamefanyika Agosti 5, 2023 huku zaidi ya wahitimu 260 wakiagwa wakiwa tayari kwa ajili ya kujiari na kuajiriwa kutokana na ujuzi mkubwa walionao.
Furahika Education College ni kati ya vyuo vichache vya kizazi hiki ambacho kimejikita zaidi kuwapa ujuzi maarifa wanafunzi ambao baada ya kuhitimu huwa ni chaguo kubwa kwa taasisi, makampuni na mashirika mbalimbali, kwali mbali na ujuzi wengi wana nidhamu na maadili ya hali ya juu.
Wahitimu wanaotokana na kozi za hotel management, ushonaji, computer ICT, secretarial, upambaji na urembo, tourism, cleaning and forwarding (bandari) ndiyo walioagwa.
Aidha, katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Shirikisho wa Vyuo Vikuu kupitia Chama Cha Mapinduzi, Yunus Hassan Seleman.
Mgeni rasmi huyo aliwataka wazazi kuendelea kupeleka wanafunzi Furahika Education College kwa ajili ya masomo mbalimbali ili kuweza kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chuo hicho kinatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hakuna chuo kama hicho Tanzania.
Pia, Seleman aliwaomba viongozi wa Jumuiya ya Wazazi na Jumuiya ya Vijana walete vijana mbalimbali waweze kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kujiepusha kujihusisha katika dawa za kulevya.
Sambamba na matukio ya uhalifu ukiwemo ujambazi, uzinzi na aliomba watumishi mbalimbali wa Serikali na viwanda vidogovidogo kujiunga na fani mbalimbali online ambazo zinatolewa na chuo hicho.
Amesema, kozi hizo zitawasaidia kuwajengea uwezo na ujuzi hata wale waliopo nje ya nchi au ndani kwa kuingia kwenye mfumo wa chuo hicho ambao unatoa mafunzo kupitia tovuti yao.
Seleman alisema, chuo hicho ni mfano wa kuingwa, hivyo vijana wote wanapaswa kuitumia fursa hiyo kujiongezea ujuzi.
Wakati huo huo, alitoa wito kwa mashirika ya World Vision na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kuwaleta wanafunzi chuoni hapo ili waweze kupata mafunzo ujuzi kwa kozi mbalimbali ambazo ni mkombozi katika maisha yao.
Mgeni rasmi huyo pia aliipongeza Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kipawa,Kigamboni,Temeke, Tabata,Ilala, Kariakoo, Ubungo jijini Dar es Salaam kwa namna ambavyo zinashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia katika kuwapatia vijana elimu ujuzi kwa ustawi bora wa maisha yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha, ili kujisajili na masomo online ya Chuo cha Furahika bonyeza www.furahika.or.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news