Marekani, China wataka kuyajenga upya kibiashara

BEIJING-Waziri wa Biashara wa Marekani, Gina Raimondo amewasili nchini China kwa ziara ya siku nne inayolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani.

Waziri wa Biashara wa Marekani, Gina Raimondo akilakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mji Mkuu wa Beijing na Lin Feng,Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Biashara ya Wizara ya Biashara ya Marekani na Oceania, huku Balozi wa Marekani nchini China, Nick Burns akishuhudia Agosti 27,2023.(Picha na Reuters).

Kwa mujibu wa CCTV, Waziri Raimondo akiwa uwanja wa ndege alikutana na Lin Feng, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Wizara ya Biashara ya Marekani na Oceania huku ikiwa ni safari ya kwanza ya Raimondo nchini China, kulingana na ripoti hiyo.

Raimondo alimweleza Rais Joe Biden siku ya Alhamisi alipozungumza naye juu ya ziara hiyo na ujumbe unaolenga kupunguza mivutano baina ya Taifa hilo na China.

Alisisitiza kwamba anataka kuwa na mahusiano thabiti ya kibiashara na China na msingi wa hilo ni mawasiliano ya mara kwa mara.

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng aliyekutana na Raimondo awali alisema, China inataka kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Yeye ni afisa wa nne wa ngazi ya juu wa Marekani kusafiri hadi China katika miezi ya hivi karibuni, kufuatia mjumbe maalum wa Rais Joe Biden katika mabadiliko ya hali ya hewa, John Kerry, Janet Yellen kutoka Hazina na Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken.

Mheshimiwa Gina Raimondo anatarajiwa kukutana na maafisa wa China na wasimamizi wa biashara huko Beijing na Shanghai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news