Rais Lula da Silva ataka mageuzi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

LUANDA-Rais wa Brazil, Mheshimiwa Luis Inacio Lula da Silva amerudia tena wito wake wa kufanyiwa mageuzi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Mheshimiwa Lula Da Silva alipowasili nchini Angola tarehe 24,2023.(Picha na Ricardo Stuckert/Presidência da República).

Mheshimiwa Lula da Silva ametoa wito huo katika mkutano na waandishi wa habari huko Luanda nchini Angola ambapo aliwasili usiku wa Alhamisi tarehe 24,2023 baada ya kutimiza ajenda ya siku tatu katika mkutano wa viongozi wa Brics, nchini Afrika Kusini.

Katika mkutano huo, mwaliko ulitangazwa kwa nchi sita kujiunga na kundi hilo, ikiwemo Argentina. Aidha, Mheshimiwa Rais Lula da Silva mbali na kutaka yafanyike mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pia amebainisha kwamba badala ya kuwa mdhamini wa usalama, amani na utulivu, Baraza la Usalama linaeneza vita duniani.

Amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima liendane na hali halisi ya hivi sasa duniani na kubainisha kuwa taasisi hiyo ya kimataifa imedhoofika na muundo wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haukidhi tena malengo liliyoundiwa.

Kwa mujibu wa Rais Mheshimiwa Lula da Silva katika mwaka 2023 Umoja wa Mataifa umejiweka mbali sana na mipango uliokuwa nayo mwaka 1945.

Rais wa Brazil huyo wa Brazil amekamilisha safari yake ya siku mbili nchini Angola kisha jana ameendelea na ziara yake barani Afrika kwa kuitembelea nchi ya Sao Tome and Principe ambako atahudhuria pia mkutano wa 14 wa viongozi wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kireno.

Pia Mheshimiwa Lula da Silva alielezea umuhimu wa kuwepo kwa mwelekeo chanya kati ya Brazil na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali kuanzia kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news